Skip to main content

SIRI KADHAA ZA KUFANIKIWA :



   
Mafanikio ni haki ya kila mmoja wetu na ni kitu ambacho kinawezekana kwa kila mmoja.  Watu wamekuwa wakichukuria neno mafanikio kama ajari (accident ) . Ila ukweli mafanikio siyo ajari bali ni matokeo ya misimamo yetu na misimamo yetu ni munganiko wa uchaguzi wa mambo ambayo tunayamini kuwa ndio sahihi.  Kwa maana nyingine Tunasema kwamba mafanikio ni mamzi (choice ) na siyo  nafasi.  Katika maandiko tunasema mafanikio ni neema ambayo kila mmoja wetu anakeremiwa na mungu kwa kadri anavyotumikia na kuifanyia kazi neema hiyo.  Na kila mmoja wetu amejaliwa neema hiyo na mungu hata kabla hajamuleta hapa duniani.
Kabla ya kuendelea mbele hebu tuangalie kwanza utofauti kati ya mtu mwenye kiu ya mafanikio na ambaye amekata tamaa za kufanikiwa.  Kwa maana nyingine Tunasema WINNERS  VS  LOSERS. 

1. Mshindi muda wote anakuwa ni mtatuzi wa matatizo  ( problem solver and answers  finder)  . Watu washindi na wa pambanaji katika kufikia mafanikio yao muda wote huwa ni sehemu ya kutafuta majibu na kutatua matatizo yanayowakabili.  Ila kwa mtu ambaye amekata tamaa  (losers ) wao huwa ni sehemu ya kutengeneza matatizo katika jamii. 

2. Mshindi siku zote anaongoza maisha yake kwa malengo  (plan )  Ila washindwa hubaki kuwa watu wa kugairigairi mipango yao.  Kwa maana nyingine ni watu wa siyo weza kusimamia mipango yao wenyewe.  Au kwa upande mwingine tunasema ni watu amabao wanajiongoza kwa kufuata mkumbo wa watu wengine. 

3. Mshindi katika maisha siku zote hupenda kufanya kitu kwa ajili ya watu wengine  ila walioshindwa hupenda kukatisha tamaa juu ya mambo mazuri yanayofanywa na watu wanaotumikia neema zao ipasavyo. 
Kwa maana nyingine hutumia neno kwamba hiyo siyo kazi yangu.

4.mshindi (winner) muda wote huona majibu ya matatizo wakati huo mshindwa  (losers ) yeye huona matatizo pekee. 

5.  Washindi siku zote huwa ni wale amabao wanasamehe na kusamehe wenyewe juu ya mlolongo mzima wa maisha yao. Kwa maana nyingine tunasema ni watu wasiyoweza kabisa kukaa na mambo mabaya nafsini mwao.  Washindwa  (losers ) huamini kwamba visasi ndio njia pekee ya kufikia mafanikio yao. Hawa ni watu amabao hutunza vitu ambavyo vimekwisha kupita nyuma. Kwa maana nyingine Tunasema kwamba hawa ni watu ambao kwao hawana tabia ya kusamehe na kujivika yalio mema. 

6. Mshindi siku zote  huchagua kile wanacho Sema kwa upande mwingine tunasema huchanganua . Wakati huo mshindwa husema kile walichochagua bila kuchanganua. 

7. Mshindi yeye jambo hili ni gumu lkn litawezekana wakati huo mshindwa  ( losers ) yeye anasema jambo hili linawezekana ila ni gumu.

8. Mshindi siku zote hufanya kitu ili kitokee na mshindwa husubiri kitu kitokee. Kwa namna nyingine ni mtu anayesubiri miujuza itokee ili afanikiwe katika maisha yake.  

Hiyo ni badhi ya tofauti chache ambazo pia zitakusaidia kujiPima upo katika kundilipi hasa katika upande wa kupigania ndoto zako.
Ili uweze kufanikiwa katika maisha yako kuna siri kadhaa za kupitia na ambazo zitakufanya uwe tofauti katika jamii. 
1. Jiamini kuwa unaweza kufikia malengo yako.  Kujiamini na kuamini ni moja ya siri kubwa katika kufikia mafanikio yako. Usipokuwa na ujasiri pamoja na Imani huwezi kufikia mafanikio yako kamwe.

2. Chagua marafiki wenye maono. Jambo ambalo watu wengi hukosea ni kwenye uchaguzi wa marafiki katika maisha yao. Rafiki ana msukumo mkubwa katika kubomoa ndoto zako au kukusogeza mbele kimafanikio.   
Kwa mfano unachagua marafiki ambao hutumia muda mwingi kujadili anasa  kwamwe hawawezi kukusaidia katika kufika kule ulikokusudia. 

3. Tengeneza mipango sahihi  (plan). Huwezi kufanikiwa kwa kutaka kufanya mambo yote kwa wakati mmoja.  Maana ya kuweka mipango ni kukusaidia kuweka kipaumbele katika mambo ya msingi.  Ukisema uendeshe maisha bila mipango lazima uataona kipato chako ni kidogo na hakitoshi kukufikisha u endapo. 

4. Jifunze kuheshimu fedha.  Kwa maana nyingine Tunasema lazima uwe na nidham ya kuitumia pesa.  Kuna watu ambao kwao pesa hazikai kwenye akaunti zao . Hawa ni watu ambao wanapenda starehe ambazo majuto yake ni makubwa kwa badaye.
5. Jenga ukomavu wa fikira 
Fikira chanya ni nyenzo thabiti katika kufikia mafanikio yako.  Kuwa mtu wa kutafuta maarifa na ujuzi uliosahihi kupitia kusoma vitabu au njia yoyote iliosahihi.

Hizo ni badhi ya siri kadhaa za mafanikio  japo zipo nyingine nyingi.  
Ili kuendelea kupata makala nyinginezo,  endelea kuifanya blog hii kuwa sehemu yako ya maarifa. 
Share makala hii katika marafiki zako kwenye mitandao yote ya kijamii ili na wao tuweze kwenda sambamba

Watu wasiyo kuwa na malengo mara nyingi hupenda sana kutumia maneno haya

1)Sina mtaji
2)Sina Connection
3)Nitaanza rasmi kesho
4)Mimi ni wa hivihivi tu
5)Mifumo mibovu ya Serikali ndiyo inayonirudisha nyuma
6) Mke/mme/ndugu zangu Ndiyo walioniangusha/kunitenda/kikwazo
7)Kupata ni majaliwa
8)Usilazimishe mambo
9)Kuna watu special siyo mimi.
10)Sina bahati
11) kupata si uhodari nami nitapata tu.
12) Mimi ni fungu la kukosa tu.
13) muda wangu bado nitapata tu
14) mungu hajapanga hata vidole mkononi havilingani.
15) wapo waliopangiwa sisi wasindikizaji
16) Familia yetu hakuna tajiri nianze mimi?
17) hata wanaotafuta mbona wapo vilevile...fulani namjua mbona yupo tu kama mimi au namzidi.
18)Rais anabana sana

Comments

Popular posts from this blog

MAMBO YANAYO KWAMISHA UFUGAJI

MAGWEIGA POULTRY INVESTMENT(wajasiriamali wa kuku na bidhaa zake) MAMBO YANAYOKWAMISHA WAFUGAJI WENGI.  Ufugaji ni rahisi ukitumia faida za mezani na kushuhudia watu wanafanya.  Hali hi inaweza ikawa tofauti ukianza wewe mwenyewe kwa vitendo.  Ni jambo gumu kiasi chake endapo mfugaji atapuza kanuni bora za Ufugaji.  Hapa mfugaji mpya anapaswa kujitathimini na kujipima kama anaweza kutoboa na kufikia matamanio yake kiufugaji.     Ufugaji ni kazi ngumu lakni imejawa na mafanikio kabambe na pia ni miongoni mwa furusa ambazo zipo wazi.  Ila vigezo na mashariti kuzingatiwa. kinacho kwamisha ufugaji kwa asilimia kubwa ni mambo yafuatayo . Mfugaji asipo yavalia njuga ataishia kwenye msongo wa mawazo na kujipa magonjwa ya moyo. Magweiga poultry investment 1. Magonjwa . Kipengele hiki kimekuwa changamoto kubwa sana kwa sisi wafugaji.  Yapo magonjwa changizwa  ambayo ni mfugaji mwenyewe anakubaliana na ugonjwa husika kutokea  ✔️ Typhoid...

KUWA NA MSIMAMO KWENYE MAISHA YAKO

Ulishawahi kujiuliza ni  kwanini watu wachache wanafanikiwa katika maisha huku wengi wakibakia masikini?  Ukweli ni kwamba sio kuwa wao wanasiri nyingi za kufanikiwa kuliko wewe bali ni misimamo thabiti waliojiwekea ili kuendana na ukuaji wa changamoto za maisha. Ni watu ambao wanafikiria vitu na mambo makubwa na kufanya vitu hivyo kwa msimamo bila kukubali kushindwa.  James William  (Harvard University ) aliwahi kusema kwamba " A human being can alter their lives by altering their attitude of mind" akiwa anamanisha kwamba binadamu yeyote anaweza kupunguza maisha yake kwa kupunguza musimamo wa fikira zake. Duniani kote utafiti unaonyesha kwamba rasirimali watu ndio nyenzo muhimu sana katika biashara yoyote yenye mulengo wa mafanikio.  Ila rasilimali hiyo ndio imekuwa ikipotea kila siku kutokana na watu kukoswa msimamo  (atttitude) Watu wanaweza kuwa asset kubwa sana katika maisha yako. Mafanikio yoyote hayapimwi kwa kipato ulichonacho bali pia ...

USIWE NA TAMAA KATIKA UFUGAJI.

  MADHARA YA TAMAA KATIKA UFUGAJI  Mfugaji yoyote ili aweze kuona faida ya ufugaji wake lazima aweke Tamaa pembeni.  Kuna utofauti kati ya Mfugaji mwenye Malengo na Mfugaji mwenye Tamaa.  Mfugaji mwenye Malengo hufanya muradi wake kwa uchache na kwa ufanisi, pia huweka ukomo wa kumiliki kuku kwa kiwango ambacho huweza kuwamudu na kumletea faida  Mfugaji mwenye Tamaa yeye kwake ukienda utakuta ana kuku 500 wa rika tofauti tofauti ambao hata kuwalisha ni mtihani kwake ila shida yake aonekane anamiliki kuku wengi japo faida yake ni 0%% Mfano : umeweka kuku 100 kroila  na umewakuza kwa shida hadi kufikia kutaga . Wanapoanza kutaga ni muda wa kuvuna mayai ili kurudisha garama zako.  Cha ajabu hapa utakuta Mfugaji anakurupuka kuingiza vifaranga wapya 200 kwa kutegemea hawa kuku 100 wahudumie vifaranga 200  hadi kufikia kutaga.   Pia hao kuku 100 wajiendeshe wao wenyewe kupitia mayai.  pia kuku 100 wahudumie familia. Ukweli ni kwamba itafi...