EPUKA SANA STAREHE KUWA CHANZO CHA MAUMIVU KWA YULE UMPENDAYE :
Ni jambo moja kuwa mzinzi, ni jambo moja kumsaliti mke/mume wako ni jambo moja kudharau na kutokujali hisia zake. Lakini unapata nini hasa kwa kumuonyesha dhahiri madhambi yako? Kama unafuraha kuwa unachepuka kwanini usifenye huko huko mpaka uchukue na Video za unachokifanya au hata wewe huamini kua una furaha unataka ushahidi?
Kuna haja gani ya kupiga picha na mchepuko wako? Kuna haja gani ya kutumiana sehemu zenu za uchi, kuna haja gani ya kupokea simu ya mchepuko mbele ya mpenzi wako. Wewe si umeshaamua kufanya starehe, kama kweli una furaha kwanini usifurahi peke yako, kwanini umuonyeshee, kwanini ubakize mameseji ili aje ayaone.
Kumbuka unaweza kumuomba msamaha, anaweza kukusamehe kwakua anakupenda au kwakua hana sehemu nyingine ya kwenda lakini kamwe hawezi kusahau. Kwanini starehe zako ziwe maumivu kwa wengine. Tuseme basi umemchoka na unataka kumuacha, kwani ukimuacha kwa wema bila kumuuliza kwa mapicha na dharau utapungukiwa nini? Kumbuka wewe ni binadamu, kuna leo na kesho, acha kutengeneza kesho ya visasi!

Comments
Post a Comment
asante kwa kuichagua tujengane media kuwa sehemu yako ya kujifunza