Skip to main content

NG'AMUA HAYA NA UCHUKUE HATUA KABLA YA YEYE KUFANYA HIVYO

DALILI ZA MTU ANAYETAKA KUKUACHA.
.
Sio kila mtu ana uwezo wa kukufata au kukupigia simu na kukuambia live kuwa hakutaki, muachane, wengi hawawezi kuwa kauzu hivyo na kuamua kutumia njia zingine ambazo kwa kiasi kikubwa zitakuumiza, kutesa, au kusababisha malalamiko/ugomvi unaoweza mpa sababu ya kuachana na wewe.
Zifuatazo ni dalili za mahusiano yanayokaribia kufa.
.
1: MABADILIKO YA TABIA: Mara nyingi mtu anapokua amekuchoka huwa anaanza kujenga tabia za ajabu ajabu, ambazo zitakufanya ukose usingizi, ukose raha ya maisha au hata kusababisha mitafaruku ya mara kwa mara. Mfano: Usaliti wa mara kwa mara na muda mwingine ni wa wazi wazi, gubu, kisirani, kukosoa kosoa bila sababu, kuchelewa kurudi, jeuri, dharau*kejeli, kukupiga mara kwa mara.
.
2: KUPUNGUZA MAWASILIANO: Hii ndo huwa jambo kubwa hasa kwa wenye mahusiano yaliyo nje ya ndoa na ndani ya ndoa. Mlizoeana kuchat asubuhi mpaka usiku, kupigiana simu mara kwa mara. Lakini ghafla unaona ile kasi inapungua, story, ushauri, vichekesho, alivyokuwa akikupa wakati wa maongezi yenu unashangaa vinakufa ghafla. Message mbili anakuaga, hakuna kuchekeshana, wala kushauriana.
.
3: KUTOKUPA KIPAUMBELE: Hiki ndo kipindi ambacho utampigia mara 10, utapokelewa mara moja. Utatuma message WhatsApp hata kama yuko online, hatojibu kwa wakati. Usishangae kukawa na party, na usialikwe.
.
4: KUONGEZEKA KWA VISINGIZIO: Mara nyingi mtu anapokuchoka huwa anakosa hamu ya kuongea, kuchat, kuonana, kula, hata kukaa na wewe. Usishangae sana mumeo kuanza kila akirudi nyumbani kukwambia "Anh nimeshiba", "Nimechelewa kurudi, kazi nyingi", au mpenzi wako "Baby sijaja mama alinituma sehemu ", "Dah mishe zinabana ndomana sijakutafuta".
.
5: KUTOKUJALI TENA: Hiki ndo kipindi ambacho unaongea na mkeo, yeye anakupa mgongo. Ule usile, utosheke chumbani usitosheke, ulale usilale, uumwe usiumwe, wala hana muda na wewe.
.
6: KUFA KWA UPENDO&MAHABA: Utaanza kuona mabadiliko, zile nakupenda, kusifiana, kucheza pamoja, kulishana, mabusu motomoto, kubebana, kudekezana, kutoka wote pamoja, kucheka pamoja, kula pamoja, mechi za kufa mtu, vyote utaona vinapungua kimoja baada ya kingine.
.
7: MABADILIKO KWENYE TENDO LA NDOA: Mara nyingi mtu anapoanza kujenga chuki dhidi yako, huwa anaanza kukosa hamu/hisia juu yako. Hivyo hata kama hana michepuko, huwa anakosa ile hamu ya kufanya na wewe tena. Lakini kama anayo michepuko, huwa anamaliza hamu zake huko huko, wewe unawekwa kando, au hata mkifanya inakuwa kama kajilazimisha kufanya, hivyo anaweza akaishia njiani kutokana na uchovu alionao baada ya kuhudumia michepuko, au kutokana na kukosa hamu ya kufanya na wewe.
.
Tutaendelea na uchambuzi. .......

Comments

Popular posts from this blog

MAMBO YANAYO KWAMISHA UFUGAJI

MAGWEIGA POULTRY INVESTMENT(wajasiriamali wa kuku na bidhaa zake) MAMBO YANAYOKWAMISHA WAFUGAJI WENGI.  Ufugaji ni rahisi ukitumia faida za mezani na kushuhudia watu wanafanya.  Hali hi inaweza ikawa tofauti ukianza wewe mwenyewe kwa vitendo.  Ni jambo gumu kiasi chake endapo mfugaji atapuza kanuni bora za Ufugaji.  Hapa mfugaji mpya anapaswa kujitathimini na kujipima kama anaweza kutoboa na kufikia matamanio yake kiufugaji.     Ufugaji ni kazi ngumu lakni imejawa na mafanikio kabambe na pia ni miongoni mwa furusa ambazo zipo wazi.  Ila vigezo na mashariti kuzingatiwa. kinacho kwamisha ufugaji kwa asilimia kubwa ni mambo yafuatayo . Mfugaji asipo yavalia njuga ataishia kwenye msongo wa mawazo na kujipa magonjwa ya moyo. Magweiga poultry investment 1. Magonjwa . Kipengele hiki kimekuwa changamoto kubwa sana kwa sisi wafugaji.  Yapo magonjwa changizwa  ambayo ni mfugaji mwenyewe anakubaliana na ugonjwa husika kutokea  ✔️ Typhoid...

KUWA NA MSIMAMO KWENYE MAISHA YAKO

Ulishawahi kujiuliza ni  kwanini watu wachache wanafanikiwa katika maisha huku wengi wakibakia masikini?  Ukweli ni kwamba sio kuwa wao wanasiri nyingi za kufanikiwa kuliko wewe bali ni misimamo thabiti waliojiwekea ili kuendana na ukuaji wa changamoto za maisha. Ni watu ambao wanafikiria vitu na mambo makubwa na kufanya vitu hivyo kwa msimamo bila kukubali kushindwa.  James William  (Harvard University ) aliwahi kusema kwamba " A human being can alter their lives by altering their attitude of mind" akiwa anamanisha kwamba binadamu yeyote anaweza kupunguza maisha yake kwa kupunguza musimamo wa fikira zake. Duniani kote utafiti unaonyesha kwamba rasirimali watu ndio nyenzo muhimu sana katika biashara yoyote yenye mulengo wa mafanikio.  Ila rasilimali hiyo ndio imekuwa ikipotea kila siku kutokana na watu kukoswa msimamo  (atttitude) Watu wanaweza kuwa asset kubwa sana katika maisha yako. Mafanikio yoyote hayapimwi kwa kipato ulichonacho bali pia ...

USIWE NA TAMAA KATIKA UFUGAJI.

  MADHARA YA TAMAA KATIKA UFUGAJI  Mfugaji yoyote ili aweze kuona faida ya ufugaji wake lazima aweke Tamaa pembeni.  Kuna utofauti kati ya Mfugaji mwenye Malengo na Mfugaji mwenye Tamaa.  Mfugaji mwenye Malengo hufanya muradi wake kwa uchache na kwa ufanisi, pia huweka ukomo wa kumiliki kuku kwa kiwango ambacho huweza kuwamudu na kumletea faida  Mfugaji mwenye Tamaa yeye kwake ukienda utakuta ana kuku 500 wa rika tofauti tofauti ambao hata kuwalisha ni mtihani kwake ila shida yake aonekane anamiliki kuku wengi japo faida yake ni 0%% Mfano : umeweka kuku 100 kroila  na umewakuza kwa shida hadi kufikia kutaga . Wanapoanza kutaga ni muda wa kuvuna mayai ili kurudisha garama zako.  Cha ajabu hapa utakuta Mfugaji anakurupuka kuingiza vifaranga wapya 200 kwa kutegemea hawa kuku 100 wahudumie vifaranga 200  hadi kufikia kutaga.   Pia hao kuku 100 wajiendeshe wao wenyewe kupitia mayai.  pia kuku 100 wahudumie familia. Ukweli ni kwamba itafi...