Skip to main content

Posts

Showing posts from November, 2021

USIWE NA TAMAA KATIKA UFUGAJI.

  MADHARA YA TAMAA KATIKA UFUGAJI  Mfugaji yoyote ili aweze kuona faida ya ufugaji wake lazima aweke Tamaa pembeni.  Kuna utofauti kati ya Mfugaji mwenye Malengo na Mfugaji mwenye Tamaa.  Mfugaji mwenye Malengo hufanya muradi wake kwa uchache na kwa ufanisi, pia huweka ukomo wa kumiliki kuku kwa kiwango ambacho huweza kuwamudu na kumletea faida  Mfugaji mwenye Tamaa yeye kwake ukienda utakuta ana kuku 500 wa rika tofauti tofauti ambao hata kuwalisha ni mtihani kwake ila shida yake aonekane anamiliki kuku wengi japo faida yake ni 0%% Mfano : umeweka kuku 100 kroila  na umewakuza kwa shida hadi kufikia kutaga . Wanapoanza kutaga ni muda wa kuvuna mayai ili kurudisha garama zako.  Cha ajabu hapa utakuta Mfugaji anakurupuka kuingiza vifaranga wapya 200 kwa kutegemea hawa kuku 100 wahudumie vifaranga 200  hadi kufikia kutaga.   Pia hao kuku 100 wajiendeshe wao wenyewe kupitia mayai.  pia kuku 100 wahudumie familia. Ukweli ni kwamba itafi...

VITU MUHIMU KWA VIFARANGA 100

 Mahitaji Muhimu kwa vifaranga 100  ndani ya wiki 3 mpaka 4. www.tujenganemedia. blogspot. Com ✔️ chakula 50kg statar. Huweza kutumika kwa wiki 3 kisha ukaongeza kiroba kingine  ✔️ chungu joto 1 au bulb joto kwajili ya vifaranga 1 ✔️ vyombo vya maji 3 ✔️vyombo vya kulishia vifaranga 3 mpaka 4 . Hi unaweza kutumia mifuniko yenye muundo wa masinia.  Dukani ipo.  ✔️ Dawa ya kuanzishia  ( NEOXCHICK FORMULA ) ✔️ glucolin  kwajili ya kuwapa kwa masaa matatu ya mwanzo.   ✔️ Maranda ya mpunga au matandazo kwajili ya kufyonza vinyessi vyao.   ✔️Trimizine : hi tunachanganya kwenye neochick ili kusaidia vifaranga wasipate magonjwa ya kuhara kama vile typhoid ndani ya siku 7 mapaka 14   Hayo ni acheche katika mengi ambayo mfugaji unapaswa kufanya katika muradi wako.  By Bahati MagweIgarashi 0757472165 0786155188  Vifaranga wa siku 1 ni 1500/= Vifaranga wa mwezi  5000/=    Karibu Sana 

MAHITAJI MUHIMU KABLA YA KUWEKA VIFARANGA BANDANI.

 MAHITAJI  MUHIMU KABLA YA KUWEKA VIFARANGA BANDANI : Unapotaka kuanza ufugaji wowote wa kuku lazima uwe na mahitaji muhimu ya kusaidia muradi wako ukuwe vyema na kuepukana na changamoto.   Miongoni mwa mambo muhimu ni kama vile.  1. Banda kulingana na idadi ya vifaranga unavyotaka kuweka.  Usizidishe vifaranga katika banda moja ili kuepusha ukuaji hafifu na matatizo mengine kama vile kudonoana.  Hakikisha banda limezingatia kanuni zote za ujenzi ikiwemo  ✔️uelekeo wa upepo  ✔️upauwaji wa paa ✔️uelekeo wa maji yani lisiwe katika mkondo wa maji  ✔️Hewa iingie na kutoka kwa usahihi ili kuzuia mambukizi zaidi ya magonjwa pale yanapokuwa yametokea.  2.  Vyombo vya chakula na maji kulingana na Idadi sahihi ya vifaranga.  Kwa mfano vifaranga 100 wanahitaji Vyombo 3 vya maji na vitatu vya chakula ndani ya siku 30 mpaka 45 3. Vyungu joto au taa za umeme za kulelea vifaranga  4. vitaru vya kulelea vifaranga endapo banda ni kub...

UPANGILIO WA CHANJO KWA VIFRANGA.

MPANGILIO SAHIHI WA CHANJO KWA VIFARANGA CHOTARA NA KIENYEJI ............................................. Vifaranga ili wakuwe vyema na kusitawi ni lazima wazingatiwe katika chanjo na chakula bora.   Chanjo humsaidia kifaranga kujikinga na magonjwa hatari ambayo hayana dawa kama vile mdondo,  mahebe  ,  Gumboro na ugonjwa wa ndui.  Haya ni magonjwa ambayo yakitokea Katika shamba huweza kuleta vifo na hasara kubwa kwa mfugaji.   Magonjwa haya huwa yana chanjo na sio dawa hivyo mfugaji anapaswa kuzingatia ratiba za chanjo kwa usahihi     *RATIBA ZA CHANJO*  SIKU 1.    MAREK'S SIKU 7.    NEWCASTLE SIKU 14.    GUMBORO SIKU 21   NEWCASTLE SIKU 28   GUMBORO SIKU 35     NDUI Katika hizo chanjo , chanjo mbili hutolewa kwenye bawa ambazo ni chanjo ya marekes  na  chanjo ya ndui.  Chanjo zilizobakia huchanganywa katika maji Kwa maelekezo sahihi ya kitaalamu....

USIMAMIZI WA KUKU WANAO TAGA.

 SABABU ZA KUJIENDESHA KIHASARA KATIKA UFUGAJI Ufugaji ili ukuletee matokeo chanya inakutaka mfugaji utumie akili nyingi na mbinu sitahiki . Kuliko matumizi mengi ya pesa akili kidogo  ( maarifa ) Nimewahi kusema huko nyuma Kwamba kabla hujaweka pesa zako kwenye tasinia ya ufugaji inakuhitaji kwanza uwekeze kwenye upatikanaji wa Elimu sahihi kuhusu ufugaji.  Kinyume cha hapo ni kuhatarisha mtaji wako. Wapo watu wanaingia kwenye tasinia hi ya ufugaji kwa sababu wanapesa.  Ukweli usiopingika ni kwamba pesa haiwezi kuzuia kuku kufa isipokuwa maarifa sahihi ya ufugaji ndio yatakusaidia kujua 👇 ✔️ Anaumwa nini  ✔️Atumie dawa gani  ✔️Kwa nini Anaumwa  ✔️ dozi sahihi kwa ugonjwa alionao  ✔️Ataweza kupona?  ✔️Anaweza kuambukiza wengine  ✔️Ni magonjwa yatokanayo na ukosefu wa chanjo au mazingira wanayoishi? ? Ukisema unafuga kwa sababu unapesa itakusaidia kuzuia magonjwa kwa kununua madawa sio kweli kwa sababu kuna kipindi inafikia kuku wanagoma...

KANUNI MOJA MUHIMU KATIKA UFUGAJI.

Kanuni ambayo wafugaji wengi hawajui na ambayo inatumiwa sana na kuku chotara wanaotaga ni Ile kanuni ya NIPE NIKUPE kanuni hi hutumiwa sana na binadamu kwenye biashara lakini ndio kanuni maarufu Kwa ufugaji.  Kuku chotara anaitumia sana hi kanuni kwamba Ukinipa kibovu nitakupa kibovu ila Ukinipa kilicho bora na mimi nitakufuta machozi kwa kukupa bora zaidi.   Hapa kuku hawa humanisha kwamba ukiwapa huduma nzuri ya chakula +maji + mabanda safi watakupa mayai mengi na bora zaidi  Pia ukiwapa chakula dhaifu watakurudishia udhaifu wako kwa kukupa mayai machache na yalio dhaifu.  NIPE NIKUPE  ijue hi kanuni mfugaji itakusaidia sana.    By magweiga 📞+255757472165 📞+255786155188 Karibu kwa huduma ya vifaranga walio bora wa kroila wa siku 1 kwa shilingi 1500 /=   Tupo kibaha  pwani

ULEAJI WA VIFARANGA NDANI YA SUKU 30 ZA MWANZO

 MAANDALIZI KWAJILI YA  VIFARANGA  NA MAMBO  MUHIMU SIKU 30 ZA MWANZO.          By Magweiga  bahati bahatichacha698@gmail.com 📞+255757472165 📞+255786155188 ukitaka kuwa mfugaji mzuri na mwenye kujenga uzoefu mzuri katika ufugaji huna budi kuanza na vifaranga.  Changamoto mbalimbali za uleaji wa vifaranga ndio uhalisia wa kuku katika magonjwa, ukuaji na mambo mengine yanayo mhusu.  Upo utofauti mkubwa wa uelewa kati ya mtu ambaye ameanza kumfuga kuku tangu kufaranga hadi kutaga kisha kuuzwa  na yule ambaye ameuziwa kuku wakiwa wakubwa.   Aliyeuziwa kuku wakubwa anakuwa na changamoto chache za kutatua kuliko yule mkuzaji wa huyo kuku tangu kufaranga.  Hata katika uchambuzi wa changamoto zinazohusiana na kuku Anakuwa na uwanja mdogo wa kuzungumzia kuku kiundani.  Asilimia kubwa ya watu hupenda kuwa wafugaji lakini hawataki kupita katika mchakato wa kulea vifaranga.  Wengi huamini kukuza vifaranga ni...