Skip to main content

Posts

Showing posts from May, 2018

ZINGATIA HAYA UNAPOKUWA MBALI NA MWENZI WAKO

KAMA UKO MBALI NA MPENZI WAKO ZINGATIA HAYA Kama unaishi mbali na mpenzi wako kwanza kabisa unatakiwa kukubali kua mko mbali, huwezi na wala hutakiwi kucontrol kile anachokifanya kule, acha kufuatilia anafanya nini huko, yuko na nani na mambo kama hayo, kwa kfuupi wivu weka pembeni kwani ukiendekeza utachanganyikiwa. Kuna mambo mengi atayafanya mazuri na mabaya lakini kama hakuonyeshei basi huna haja ya kuyafukunyua. Jambo la pili ni mawasiliano haya ni muhimu na anapokupigia simu au unapompigia tumieni muda wenu vizuri kwa kuongelea kuhusu mapenzi na si kila siku “Mbona hukupokea simu yangu? Mbona nilikuona online hukujibu SMS zangu? Kulalamika sijui nimesikia hivi? Nimesikia vile!” Atakuvumilia kwa muda kisha itaboa na atakua anakwepa kuzungumza nawe na mwisho mapenzi yatakufa. Hata kama mnaongea dakika tano zifanyeni ziwe tamu zihusu mapenzi na si kuzozana mpaka mtu akitaka kupiga simu anawaza hivi nikiongea naye si kelele tu, hakuna mtu anapenda kupigia simu mtu aliyenuna....

SIMLIZI YA KWELI YA WANANDOA WAWILI MARRY NA JOSEPH

Mkasa wa kweli wa  wanandoa fulani  ambao mpaka Mwisho wa simulizi hii kila mwanandoa ukiweza kupata Muda wa kusoma utajifunza kitu. Usiwe Mvivu wa kusoma mkasa huu   JE NANI ALAUMIWE KATI YA JOSEPH NA MARRY? Ongozana nami mpaka mwisho wa simulizi. 1.Sehemu ya Kwanza Joseph Alimuoa marry Kati ya mabint waTatu aliowahi kuwa nao,  marry Alikuwa mzuri sana hata  wa sura kiasi Kwamba Joseph akavutiwa naye Bila kujua uzuri wa mke ni tabia  na sio sura wala shepu,lakini Joseph Alikuwa amekufa ameoza kwa marry, Maisha ya ndoa yakaanza wakiwa hawana kitu yaani wote ndio Wanaanza from zero,  walikaa Muda kidogo Bila kupata watoto baadaye Mungu akawasaidia wakapata mtoto na familia ikaongezeka,  Joseph Alikuwa ni mtoto wa kwanza kwao na Alikuwa ametoka familia ya Kimaskini sana na marry pia hivyo hivyo tena kwao na marry ndio kulikuwa zaidi  Baada ya miaka kazaa Mke akaanza kabadilika tabia mke akaanza kuwa Mchoyo ndugu wakija Nyumbani an...

MAFANIKIO HUANZA NA FIKIRA.

                                            MAFANIKIO HUANZA NA FIKIRA Nimependa kushare nanyi kidogo baada ya kufanya utafiti ambao sio rasmi saana, hasa tukizungumzia mada ya Mafanikio. Watu wengi hasa sisi vijana tumekuwa tukichukulia mafanikio kama tukio....(Success as an event) lakini ukweli ni kwamba mafanikio au Kufanikiwa katika jambo lolote ni Mchakato(a process) ambao unakuwa na Mkakati Fulani/ Maalumu (strategy). Mchakato huo maalumu lazima uanzie akilini kwanza. Tunapoongelea Mafanikio katika chochote ni lazima kwanza kuamini katika kufanikiwa ndipo tuandae mkakati ambao utakusaidia au ambao utakuwa ndio njia ya kukufikisha kwenye Mafanikio. Ukweli ni kwamba Huwezi yafikia Mafanikio Makubwa yoyote halali yenye Thamani Bila Kuamini kwanza katika Mafanikio na kujenga mtazamo Chanya juu ya kile unachokiendea. Lakini Kwa Kumalizia Unaweza kuamini katika Mafaniki...

KUWA NA MSIMAMO KWENYE MAISHA YAKO

Ulishawahi kujiuliza ni  kwanini watu wachache wanafanikiwa katika maisha huku wengi wakibakia masikini?  Ukweli ni kwamba sio kuwa wao wanasiri nyingi za kufanikiwa kuliko wewe bali ni misimamo thabiti waliojiwekea ili kuendana na ukuaji wa changamoto za maisha. Ni watu ambao wanafikiria vitu na mambo makubwa na kufanya vitu hivyo kwa msimamo bila kukubali kushindwa.  James William  (Harvard University ) aliwahi kusema kwamba " A human being can alter their lives by altering their attitude of mind" akiwa anamanisha kwamba binadamu yeyote anaweza kupunguza maisha yake kwa kupunguza musimamo wa fikira zake. Duniani kote utafiti unaonyesha kwamba rasirimali watu ndio nyenzo muhimu sana katika biashara yoyote yenye mulengo wa mafanikio.  Ila rasilimali hiyo ndio imekuwa ikipotea kila siku kutokana na watu kukoswa msimamo  (atttitude) Watu wanaweza kuwa asset kubwa sana katika maisha yako. Mafanikio yoyote hayapimwi kwa kipato ulichonacho bali pia ...

KUJITAMBUA KATIKA WAKATI SAHIHI

Kujitambua katika maisha ni moja ya hatua kubwa ambayo humtofautisha mtu na mtu katika swala zima la mafanikio. Nini maana ya kujitambua? Ukizungumzia neno kujitambua kwa mtu yeyote ni  kuwa mtu sahihi, mahali sahihi, kwa muda sahihi.   Kuwa mtu sahihi maana yake ni kuwa mtu ambaye unajisimamia na kutekeleza kile ambacho unatakiwa kufanya wewe kama mwanadamu. Mahali sahihi inamanisha kwamba upo kwenye kiwango ambacho ulistahiri kuwepo kimaisha kwa maana ya kwamba kiuchumi, kijamii na hata kisiasa.  Asilimia kubwa ya vijana waliowengi hupoteza uelekeo wao wa maisha kwa kushindwa kujitambua katika umuri nyeti ambao bado vijana hawa wanakuwepo na nguvu za kutosha za kuwawezesha kushughulika na ndoto zao katika maisha.  Tunapaswa kujitambua na kutambua kwamba chochote ambacho kinaonekana sasa katika Macho yetu ni mamzi mugumu yaliofanywa na watu kama sisi.  Vijana wengi tumekuwa na tabia furani ya kuiambia dunia tunachokifahamu badala ya kuonyesha Dunia unach...

NAFASI ZA KAZI

*NAFASI ZA AJIRA SHIRIKA LA REDCROSS TANZANIA* • MADEREVA wanahitajika-Sifa Leseni ya Udereva • waliosomea Community Development- Wanahitajika • Waliosomea WATER ENGINEERING/Water and Sanitation • SOCIAL WORKERS JOBS/ Community Development *Deadline May 8,JINS YA KUTUMA MAOMBI HII HAPA*👉👉http://www.unistoretz.com/magazine/job-opportunities-at-tanzania-red-cross-society/ ————————————————— *NAFASI 104 ZA KAZI TANESCO- DAR NA MIKOA MINGINE(INTERNAL ADVERT)* • Ajira kwa walio na cheti cha Form Four •AJIRA kwa walio na Certificate/Diploma • Nafasi za Ajira kwa Degree Graduates *BOFYA HAPA KUFAHAMU ZAIDI* 👉👉http://www.unistoretz.com/magazine/103-job-vacancies-at-tanzania-electric-supply-companytanesco/ ———————————————— *NAFASI ZA KAZI NGORONGORO CONSERVATION* 👉👉http://www.unistoretz.com/magazine/job-opportunity-at-ngorongoro-conservation-area-authority-ncaa-manager-community-development/ ————————————————— *NAFASI ZA KAZI STANDARD BANK TANZANIA* • Graduates...

KUWEKA AKIBA.

Ukiwa na malengo ya kutimiza katika maisha yako inakulazimu kuweka akiba zaidi ya kuendekeza starehe ambazo hukugarimu kiasi kikubwa cha fedha.  Jambo kubwa la kuangalia hasa unapokuwa unania ya kufikia ndoto zako ni mugawanyo sahihi katika mambo yaliosahihi kwa wakati sahihi.   Asilimia kubwa ya watu hushindwa kufika kule wanako kusudia kutokana na kukoswa msimamo wa kuweka akiba na kujizuia katika mambo yasiokuwa na tija Inatakiwa kuwa na mugawanyo mzuri wa matumizi yako ili  uweze kubakiza asilimia 10% ya kipato chako kama akiba.  Endelea kufuatilia makala hizi kupitia blog hii  huria.  Tunakwahidi kuendelea kukupa makala ambazo zimesheheni maudhui muhimu katika kukujenga kifikira.  Usisahau maoni yako ni ya muhimu sana katika kujenga kifikira.   KANUNI UNAZOTAKIWA KUZINGATIA KUHUSU FEDHA. Zipo kanuni mbalimbali ambazo unapaswa kuzingatia katika maswala ya fedha.    *KANUNI NO. 1*  Kamwe usikope fedha...

TANGAZA NASI BIASHARA ZAKO

Tangaza nasi kupitia blog yako ya tujengane media  muda wowote bila vikwazo. Tutafikisha matangazo yako zaidi ya nchi 108 Duniani kote. Kuwa wa kwanza kujulikana kibiashara na kutangaza kipaji chako iwe mziki , mpira,  riadha nk. Utatangazwa kwa mwezi mzima kupitia blog hii kwa garama nafuu  kabisa.  Ili kutufikishia matangazo yako wasiliana nasi kupitia E-mail bahatimagweiga467@gmail.com  au simu namba  +255 786 9555 89. Kumbuka Huduma zetu ni ndani ya masaa 24 hakuna ukomo wa matangazo. Share na marafiki zako hasa wenye nia ya kufanikiwa kimaisha pia na wale amabao wamekwisha kujikatia tamaa hapa ndio sehemu yao sahihi.

SIRI KADHAA ZA KUFANIKIWA :

    Mafanikio ni haki ya kila mmoja wetu na ni kitu ambacho kinawezekana kwa kila mmoja.  Watu wamekuwa wakichukuria neno mafanikio kama ajari (accident ) . Ila ukweli mafanikio siyo ajari bali ni matokeo ya misimamo yetu na misimamo yetu ni munganiko wa uchaguzi wa mambo ambayo tunayamini kuwa ndio sahihi.  Kwa maana nyingine Tunasema kwamba mafanikio ni mamzi (choice ) na siyo  nafasi.  Katika maandiko tunasema mafanikio ni neema ambayo kila mmoja wetu anakeremiwa na mungu kwa kadri anavyotumikia na kuifanyia kazi neema hiyo.  Na kila mmoja wetu amejaliwa neema hiyo na mungu hata kabla hajamuleta hapa duniani. Kabla ya kuendelea mbele hebu tuangalie kwanza utofauti kati ya mtu mwenye kiu ya mafanikio na ambaye amekata tamaa za kufanikiwa.  Kwa maana nyingine Tunasema WINNERS  VS  LOSERS.  1. Mshindi muda wote anakuwa ni mtatuzi wa matatizo  ( problem solver and answers  finder)  . Watu washindi na wa pamb...

TUJENGANE MEDIA

Asante kwa kuichagua Tujengane media kuwa blog yako ya kukujuza taarifa muhimu na za kukujenga  kimaisha.  Hii ni blog ilioanzishwa kwa masirahi mapana ya kimaisha .ni blog pekee ambayo inakupa makala mbalimbali ambazo zimesheheni maudhui muhimu katika maisha yetu ya kila siku. Ukiwa na chochote ambacho kinakutatiza katika maisha yako usisite kuomba musaada wa kifikira.  Hapa ni mahara sahihi pa kukutana na watalamu mbalimbali wa maswala ya ushauri na saikolojia za wanadamu . Maoni na mibadala mbalimbali vitakuwa sehemu muhimu ya kubadilishana ujuzi,  maarifa pamoja na ukomavu wa fikira. Unachotakiwa kufanya ni kuwajulisha wenzako kujiunga katiaka blog hii. Sambaza linki hii kwa wenzio. www.tujenganemedia. blogs port. com

MAISHA YETU

                                 MAISHA Maisha ya mwanadamu yananyakati mbalimbali ambazo lazima  azipitie , hivyo uvumilivu ni jambo muhimu sana hususani katika maswala ya kujipanga kimaisha. haina maana kwamba ukishindwa eneo moja ndio umeshindwa maeneo yote katika maisha. kila changamoto unazopitia zinafunzo kubwa katika safari ya kuyafikia malengo yako. usikubali kusalenda juu ya harakati za maisha.  Nirahisi sana kukata tamaa hasa ukiwa mtu wa kufuatilia mambo ambayo hayana faida katika ubadaye wa maisha yako. kwa mfano swala la kuchezea muda kwa kujidanganya kwamba ipo siko utatekeleza pale umuri utakapokuwa umefika .  endelea kufuatilia makala zangu katika kurasa mbalimbali za mitandao ya kijamii ili tuweze kwenda sambamba katika kuyafikia malengo yetu na kutimiza ndoto zetu Pia usisite kujifunza pamoja na wenzio kupitia blog hii ambayo ni huru kwa vijana na kila mtu am...