Skip to main content

Posts

Showing posts from 2019

UTAJUAJE MTU ANAYE KUSARITI?

Kama mtu anachepuka au anakusariti lazima kutakuwa na dalili au viashiria  kadhaa kwake Dalili za kujua mtu anaekusaliti 1. mwanandoa anayetoka nje ya ndoa hana muda wa kusikiliza familia ina tatizo au furaha gani. Anafafanua kuwa hiyo inatokana na muda wote kufikiria mambo ya familia nyingine hata kama ni ya mtu huko alikoanzisha uhusiano. 2. Kuchukia kushiriki tendo la ndoa Anasema wengi wao hufanya mapenzi na wenza wao kwa kujilazimisha na wakati mwingine kulazimishwa kwa uwazi kabisa 3. mwenza anayetoka nje ya ndoa muda mwingi anakuwa mtu wa safari za ndani au za nje ya eneo analoishi. 4. anayechepuka anakuwa makini na simu zaidi ya kawaida, yupo radhi aende nayo bafuni, anakuwa makini asikamatwe anayochat kwenye simu. 5. kuchelewa kurudi nyumbani nk. Tutaendelea kuangazia dalili mbalimbali za mtu anayekusariti 5. Kuongeza upendo ghafla: mwanaume anapoanza kutoka nje yandoa, kama ndoa yake haina vurugu , anaweza kuonesha upendo mkbwa hadi mkewe akashangaa na kujiuliza....

UNACHOTAKIWA KUFANYA BAADA YA KUSARITIWA / KUKATALIWA NA MWENZI WAKO

Watu wengi hukosea katika mahusiano  kwa kutokuwa  wavumilivu pale wanapoachwa au kusaritiwa.  Wengi huwahi sana kuingia kwenye mahusiano ikiwezekana siku moja baada ya kuachwa na mpenzi wake.  Ukweli ni kwamba huwezi kupatia katika mahusiano kama hujafanyia kazi sababu na changamoto zilizo mfanya huyo mwanaume au mwanamke akukimbie .wengi husema lengo ni kuziba magepu na kupunguza stresi lakini ukweli ni kwamba baada ya mchungu kuisha utarudia makosa yale yale  ya mwanzo.  Unachotakiwa kufanya baada ya kusaritiwa au kukataliwa na mpenzi wako ni........ 1. Jitathimini kwanza 2. Jifikirie kwa kina sana ili kubaini ukweli wa kusaritiwa au kukataliwa kwako. 3. Punguza jaziba na hasira zako kwani zinaweza kukufanya ukaumia zaid pale unapo ongea na aliyekusariti. 4. Punguza kumwambia kila mtu juu ya kuumizwa kwako 5. Jitahidi kusahau . Ukizingatia hayo itakuwa rahisi sana kufika mbali kimahusiano na kufanya chaguo sahihi la mwenzi wako. Ukiendelea kuingia...
🏆🎓❤👠👇💚🖊 Uzuri wa sura pekee haukufanyi kupata tiketi ya kuimiliki ndoa kwa asilimia 100 % Bora uwe mrembo wa akili, Maarifa, unyenyekevu, Hekima, ukarimu, upendo maana hivyo vitakupa uhakika wa kuifikisha ndoa yako salama katika safari ya maisha ya ndoa mulioanza. 🍇👇🎓👫🏆 Inaleta picha gani kujiita mrembo huku unaambatana na mumeo kwenda kwenye baraza la wazee kudai ushauri wa Talaka? ?? Kisa umepata wa pembeni anaye kupenda? Uremho wako utakuwa useless kwa mume wako endapo Uremho huo utakuwa hauna ushirikiano na tabia binafsi. © *Bahati Magweiga* Mshauri elekezi wa vijana na mahusiano 💚🏆🍇 Unakutana na mabinti wazuri kweli ambao wakipita sehemu wanaume wote wanaacha kazi zao na kuanza kuulizana maswali. Wengine mpaka wanawapigia makofi kwa uzuri wao  lkn hata ukiwauliza hao wanaume kwa nn wasiowe hao mabinti???? ..........................................................................................   ✔Kila mwanaume anapiga chenga na kusema hawezi kelel...
🏆🍇🎓💚🏆👇🖊 Kwa wanawake maisha yamebadilika kwa asilimia kubwa sana. Wakati wewe unafikiria na kujivunia Elimu yako kuwa mtatuzi wa matatizo yako kwenye ndoa,  mwenzako ambaye hakwenda shule anajivunia taaluma ya mapenzi aliopata mtaani baada ya kushindwa kuendelea na masomo. 👇👇👇💚🍇🏆🖊👠 Hii imekuwa ikiwatesa wanawake wengi wasomi.  Wao wanawaza kwamba mwanaume anaweza kunaswa na pesa zake na kutulia kwenye ndoa.  Yuko tayari kumpa mwanaume mshahara wake wote ili awe na furaha katika ndoa.  Ukweli ni kwamba mshahara wako unaweza kununua vitu vingi sana kwa faida ya ndoa yako lakini sio furaha itokanayo na tendo la ndoa kati yako na mume wako. ......................................................................................... Katika mazingira kama hayo ni asilimia 100 % kumkuta yule binti ambaye alikuwa kilaza darasani kwenu anaishi vizuri kabisa katika ndoa yake na anafurahia maisha ya ndoa yake zaidi yako wewe unayelingia mshahara na Elimu. Ukw...
Moja ya kitu ambacho kinakimbiza wateja dukani kwako ni kupokea mteja huku umekaa. Kinaua mood ya wateja wengi sana. Mteja ni kama mgeni,a napokuja dukani kwako uchangamfu wako ndiyo utamfanya kununua. Hembu jiulize umeenda kwa rafiki yako, umefika anakukaribisha anakuacha sebuleni anaenda kupiga stori nnje na watu wengine utaruudi? Sasa una duka mteja anakuja umekaa, anaulizia kitu flani umekaa unamuonyeshea kwa mkono tu au unamuambia ingia uangalie! Ndugu yangu labda kama unauza Oxygen kwamba nisiponunua nitakufa sirudi. Mteja akija kwako kwanza nyanyuka huku ukimkaribisha, akiulizia nguo flani nenda ishike, hata kama hutaki kuishusha lakini mgeukie muulize ni saizi gani, kama ni sahani muulize unataka rangi gani na chochote kile. Unaponyanyuka kuna mambo mawili yanatokea, kwanza anahisi unamhehsimu, anaanza kujiona kuwa kumbe na yeye ni wa muhimu anaheshimiwa, lakini pili anaanza kuona aibu, anaona kuwa huyu nisiponunua nitakua nimemsumbua. Lakini pia kuna kitu cha tatu kinatokea ...
Mke au binti unayetarajia kuolewa lazima utambue kuwa mume wako anapokuoa pia Ana wazazi wake kama wewe na Ana ndugu zake Kama wewe, imekuwa kawaida kwa mke kutaka au kupenda na kufurahia pale Ambapo mume Wake kama Ana uwezo Kusaidia ndugu zake na wazazi wake lakini linapokuja suala La mume kutaka Kuwasaidia ndugu zake wengi huwa tunakasirika na hapo ndiyo tunaanza wengine kuonyesha rangi zetu halisi na makucha yeti, labda niwaulize kwani Kuna ubaya Gani mume akisaidia ndugu zake au wazazi wake na mbona kwenu mkisaidiwa hukatai na uwezo upo, wengine tunaenda Mbali zaidi mpaka mnachonganisha ndugu na mume wako au mume wako na wazazi wake wakati wewe ndiyo unatakiwa kuwa kiunganishi mzuri kwa ndugu wa mume wako  na wazazi tena wakati mwingine hata ukiona mume wako Anajisahau sana na kuwa bize na mambo ya familia tu ni muhimu kumkumbusha kuhusu kuwakumbuka wazazi hata kwa kuwatembelea hata kama wazazi wana uwezo pia wapelekeeni hata zawadi yoyote mtapata Baraka za wazazi pia, hata kam...
USIRUHUSU WATU KUTUMIA HISTORIA YAKO KUKUNYANYASA! Kuna mambo mengi ambayo uliyafanya kipindi cha nyuma, kuna hatua nyingi ulipitia, zipo nzuri zipo mbaya, kuna mambo mengi ambayo unatamani kuyasahau katika maisha yako lakini huwezi, kuna mambo mengi unatamani kuyabadilisha katika maisha yako lakini huwezi. Yameshatokea na ni sehemu ya maisha yako, haya tunayaita historia, si sehemu tena ya maisha yako, wewe ni mtu mpya, huwezi kubadilisha historia lakini usijihukumu au kuruhusu watu kukuhukumu kutokana na historia yako. Ulikua Malaya kweli, ulikua mwizi kweli, umetoka katika familia ya kimasikini, ulikua mshamba, ulikua unadanga, ulikua marioo na chochote kile ambacho ulikua, kama umeshapita katika hali yoyote mbaya na sasa hauko huko cha kufanya ni kuangalia historia na kumshukuru Mungu hauko kule tena. Acha kujihukumu, acha kujisikia vibaya na kubwa kabisa usiruhusu watu kukufanya ujisikie vibaya. Anaweza kuwa mume au mke, wanaweza kuwa majirani au ndugu, watataka kukudharau k...

MAMBO YANAYO CHUKIZA WANAUME KATIKA FAMILIA

Moja ya vitu ambavyo vinakera wanaume wengi ni kurudi nyumbani, unataka kuingia ndani unakuta mlangoni kumejaa wanawake, sijui majirani sijui mashoga zake mkeo wanapiga stori. Wengine wametandika na mkeka kabisa wanaongea kana bila wasiwasi wowote. Yaani ili kuingia ndani nilazima upite katikati yao. Unaingia ndani, labda mke alikupokea au hata hakukupokea lakini anatoka nnje kuendeleea na mazungumzo. Lakini pia umewahi kurudi nyumbani, umeamua ukapumzike mara hodi, mara sijui naomba hiki, mara kile mara kile. Hamkai mkapumua washakuja kuangalia TV, sijui kuna tamthilia. TV yako lakini huwezi hata kuangalia kwa uhuru, shoga yake kashikilia romoti. Mwisho wa wiki ndiyo kabisa, rafiki zake ni kujazana hapo nyumbani, wengine washenzi kabisa wanaingia na jikoni kupika. Yaani wanajifanya kupendana sana (Wale ambao wanashona na sare kabisa) wanakuja wanakaa wanapiga stori, kupika na kucheka kila saa! Mwanaume unaamua tu kulala ndani au kujifanya una ubize kzaini. Ndiyo hicho kitu k...

HISTORIA YA BAHATI MAGWEIGA

Bahati magweiga alizaliwa munamo mwaka 1993 katika hospital ya baranga wilayani nbutiama. ni miongoni mwa watoto 24 wa kuzaliwa na mzee chacha magweiga . akiwa na mama yake anayeitwa Nyakorema na baba yake chacha magweiga.  alisoma shule ya msingi baranga kisha Iramba primary school. Baada ya  hapo alichaguliwa kujiunga na sekondari NGOREME munamo mwaka 2010 kisah kuhamia kasoma sekondari iliopo majita.  baada ya kuhitimu secondary alichaguliwa kwenda kujiunga na masomo katiaka chuo cha maji kilichopo ubungo.  amehitimu cho mwaka 2017 kisha kufanya kazi kwenye tasisi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa SGR.  Akiwa chuo , bahati amefanikiwa kushika nyazifa mbalimbali ikiwemo uwenyekiti wa kamati  ya maadili ya serikali ya wanafunzi chuo , mjumbe wa tume ya uchaguzi ya serikali ya wanafunzi chuo, mjumbe wa umoja wa nchi za africa mashariki upande wa vyuo, mjumbe wa shirika la elimu UNESCO, nk.

BMB AGRIBUSNESS COMPANY LIMITED

Wasiliana nasi sasa kupata mahitaji yako ya msingi hasa katika uhitaji wa  wawanyama kama vile samamki, kuku, unguruwe pamoja na mazao mengine ya kibiashara ikiwepo nyanya , vitunguu, matikiti maji , matango nakadharika. tunapatikana kibaha katika maeneo ya fuatayo,  Mlandizi makazi mapya karibu na kijiji cha ngeta jirani kabisa na kwa diwani  maarufu kama mzee RUBWAWA, Kongowe  njia panda ya kuelekea forest mtaa wa mama MATHA pia tunapatikana soga kijijini maeneo ya kipangege  karibu na kituo na cha kupandia treni ya mwendo kasi  kilometer moja kuelekea KIPANGEGE .  hudumiwa nasi sasa ndani ya masaa 24 bila ya ufumbufu , kwetu mteja ni hadhina  kwa mawasiliano zaidi piga simu namaba 0659991953 0757472165 0752592813 au tuandikie barua pepe bahatimagweiga@gmail.com

Epuka dharau katika maisha

Kote katika njia zako za maisha utakazopita epuka kumdharau mtu usiye mjua kwa kuwa kuna nguvu furani ambayo mungu ameweka katika kila mmoja wetu. pengine ikawa ndiye mwenye mafanikio yako kwasababu tunasema kwamba mafanikio yako yako mikononi mwa mungu , pengine mungu amemuleta huyo unaye mdharau kuwa sehemu ya kufanikisha mambo yako. pengine mtu huyo ndiye yule ambaye  mungu anamtumia kama jaribu kweneye maisha yako na usipolishinda huwezi kufanikiwa hata kidogo. kuishi na watu vizuri katika jamii kutakufanya upate baraka mbele za  mungu na kutimiza makusudi maalum ambayo mungu amaeweka ndani yako ili uyatimize hapa duniani