Skip to main content

Posts

Showing posts from December, 2018

USHAURI WA WADAU WA JUKWAA LETU LA TUJENGANE MEDIA

Imeandikwa na mwanamke ambaye ameachika kwa mume wake na sasa anaishi peke yake na kulea mtoto Nimeandika kwenu  ili muweze kuelewa kuwa wakati mwingine ni vema kuwathamini Wenza wetu. Nina miaka 32, Mimi na mume wangu tulikuwa kwenye mahusiano kwa Muda wa miaka 6 na tulikuwa marafiki kabla hatujaoana, nilimsubiri mume wangu mpaka alipomaliza chuo, baadaye wazazi wakafahamiana na sisi tukafunga  ndoa na sasa tuna mtoto wa miaka 7.mume wangu Alikuwa ni mtu wa kukasirika haraka  lakini hayo yote yalianza baada ya mimi mwenyewe kutaka kumuonyesha kuwa hawezi kunitawala. Kila mara tulipogombana kidogo tu nilichukua mizigo yangu na kwenda kwetu kuelezea,dada yangu anachukua simu na kuanza kumpigia simu mume wangu na kumgombeza, na nilikuwa nikimtishia kuwa kama vipi nipe talaka yangu, huku Moyoni kiukweli simaanishi kweli kutaka talaka, nilikuwa naleta tu ufahari na kutaka kutoonekana nimeshindwa au Nina shida naye sana, siku moja kwa matendo yangu nilisababisha mpaka akan...

NUKUU KUELEKEA MWAKA MPYA

Binti yoyote  utambue kuwa kuna tofauti ya kuolewa na kujioa mwenyewe, sasa usiwe na haraka mpaka ukafikia hatua ya kuamua kujioa  maana huko ndani Jasho litakutoka, Mungu Anaweza asikupe ndizi moja Leo lakini kesho akakupa mkungu mzima wa ndizi hivyo kikubwa ni kuwa na subira na imani kwa Mungu, mfano kuchangia mahari au kujilipia mahari sio jukumu lako,  kuolewa na mtu asiye na Kazi au shughuli ya kufanya halafu weee ndio umhudumie kwa kuwa una kipato na umri unaenda na wenzio wameolewa Hilo pia hapana Hilo sio jukumu lako pia wewe ndio wa kuhudumiwa na kutunzwa pale msaada wako unapohitajika sawa ndio maana ukaitwa msaidizi na sio kichwa, kuolewa tu ilimradi na wewe umetoa gundu kuwa na mimi niliwahi Vaa shera kama wengine mnavyosema hata kama unajua kuwa mwanaume hakupendi ila una mimba yake na wazazi wamelazimisha ili usiwatie aibu Nyumbani wakati unajua kabisa ndoa yako itakuwa na mtikisiko mana mume hana upendo na wewe hivyo yajayo unayajua hilo pia sio kwakuwa kun...

WANAWAKE WENGI HUFUNGA NA KUOMBA WANAUME WA NAMNA HII.

Ndugu zangu, nimeongea kuhusu baraka na heri ya kuwa na mwanamke wa pekee pia ni vizuri kwa wakina dada na wanawake kutambua kuwa nao wanatamani sana kuwa na mume wa namna hii. Hii pia ni namna moja ya sisi wanaume kujidai katika ndoa zetu. Mke huyu ana heri anapompata mume wa namna hii: 1️⃣ Mume anayemjua Mungu na anaishi maisha ya kumpendaza Mungu. 2️⃣ Mume anayetambua kuwa yeye ni baba wa familia, mume wa ndoa na mlinzi wa familia. 3️⃣ Mume anayejua kuwa mke wake anatakiwa kusikiliza na siyo kukaripia na kugombezwa kama mtoto na wakati mwengine kutamkiwa maneno makali mbele ya watoto. 4️⃣ Mume ambaye ana uwezo wa kujishusa pale anapofanya kosa, anapoumiza hisia za mke wake. 5️⃣ Mume ambaye anatambua ulimwengu wa mwanamke na anatambua mahitaji ya mke wake. 6️⃣ Mume ambaye anashirikisha mambo ya familia na ndoa kwa mke wake na wanapanga mipango mbalimbali ya familia kwa pamoja. 7️⃣ Mume ambaye anatambua kuwa ni wajibu wake kuwa na muda wa pekee wa kuwa na mke wake, kama vile ...
Kila hatua utakayopiga kwenye maisha yako lazima itakuwa na watu wa kuzungumza juu ya hatua zako. kwa maana nyingine tunasema kwamba kadiri unavyojitahidi kufanikiwa ndivyo unaongeza kiwango cha madui kwenye maisha yako. ila idadi yao haina madhara kwako kama utaamua kupuuza kile ambacho wanakisema juu yako. wapo wengine ambao hata kama ni watu wako wa karibu lazima watajinua kuyazungumzia maendeleo yako.haijarishi umekuwa ukiwasaidia kwa kiasi gani au unawasaidia kwa kiwango gani bado hahao watakugeukia na kuwa na kuwa mwiba kwenye maendeleo yako. kinachohitajika hapo ni kuwapuza na kutofanyia kazi yale ambayo unaamini kwamba yatakuwa na matokeo hasi kwenye maisah yako binafsi. endelea kuamini kuwa mabadiliko yako yapo mikononi mwako kwa sababu tunasema kijana mpumbavu atayavunja maisha yake kwa akili zake mwenyewe. jikite zaidi kwenye kutafuta mabadiliko juu ya malengo yako na mipango yako . wanadamu siku zote wema wao huwa haupo katika yale ambayo umejitoa kwa ajili yao bali we...
Moja ya ajari kubwa ambazo nakutana nazo kila siku katika mizunguko yangu ni ajari ya watu kuvunjika moyo juu ya kile amabacho waliamini kwambacho waliamini kwamba wanakiendea kwa nia njema na lazima kukifanikisha.  Nimekuwa nikiwatia moyo watu mbalimbali ambao wamepata hizi ajari za kuvunjika moyo kwa muda mrefu.  Asilimia kubwa ya watu tunashindwa kufika kule tunakoenda kimaisha kwa sababu tumejikitia tamaa mapema au wengine tumekatishwa tamaa juu ya imani tuliyojenga kwenye kitu frani.  Hii imetugarimu wengi na kufanya tukose uwelekeo kabisa wa maisha mara baada ya kushindwa kwenye hatua furani. Leo ningependa kuchukua nafasi hii kukutia moyo tena kwamba inawezekana kufikia malengo ya kile ambacho ulikuwa unafanya na kukiacha kwa changamoto ambazo ulikuwa ukipitia.  Kumbuka kwamba hakuna aliyefanikiwa kwa kuweka kando mambo aliokuwa akiamini kwamba ni sahihi na kufanya kitu tofauti na kile kirichomo nafsini mwake. Kushindwa mara kadhaa kwenye kile unachofanya ...

NUKUU YA LEO . 9/12/2018

Kuwa na Elimu kubwa haina maana kwamba unafahamu mambo yote katika ulimwengu tunamoishi.  Asilimia kubwa ya watu wamepotea kimaisha kutokana na falsafa hasi ya kwamba wapo sahihi muda wote kwa sababu tu ya Kiwango cha Elimu alichopata darasani.  Kwa ukweli usiopingika ni kwamba umehitimu Elimu ya darasani ila bado upo wazi au mweupe kabisa kwenye Elimu ya mtaani yani Elimu inayotumika zaidi kwenye maisha.  Elimu ya darasani itakusaidia kwa uchache sana kufanikisha mambo yako ila elimu ya mtaani itakuwezesha zaidi kutimiza ndoto zako kimaisha.  Kwa mfano kuna watu wamesoma na wana elimu kubwa ila bado Elimu hiyo waliopata darasani inazidi kuwatenga mbali na jamii inayowazunguka kwa kushindwa kuchanganua mambo kwa wakati. Itikadi hii inatokana na kuaminishawa kwamba sehemu pekee itakayo kusaidia wewe kumaliza matatizo yako ni darasani.  Ila ukweli usiopingika ni kwamba darasani pekee hakutoshi kumaliza matatizo yako.  Ispokuwa hata njee ya darasani yani heki...

USHAURI KWA WATOTO WA KIKE #MSIPOTEE KABLA YA KUTIMIZA MAKUSUDI MAALIMU

JINSI BINTI ANAVYO WEZA KUEPUKA KUCHEZEWA NA KUPOTEZA NDOTO ZAKE KIMAISHA  Wakati watu wawili mwanamke na mwanaume wanapokuwa kwenye kilele cha mapenzi, ni rahisi sana kila mmoja kuchunga kauli zake na kuongea yale ambayo yatamvutia mpenzi wake ili kila mmoja awe na mvuto kwa mwenzake na hivyo kuwa karibu zaidi. Hata hivyo watu wengi (hususan wanawake) wanashindwa kung'amua kwamba, katika mapenzi kila mmoja ana lake moyoni, na ni vigumu kujua mwenzako anawaza nini juu yako. Katika mahusiano mara nyingi wanawake ndio huumizwa kwa sababu wakati mwingine mwanaume anapomtaka mwanamke humpa matarajio makubwa kuhusu hatima yao ili kumvuta, lakini kumbe analo lake moyoni na hapo ndipo mwanamke hujikuta akijitolea kwa hali na mali akijua kwamba, mwenzake amempenda na wataoana wakati kumbe mwenzie wala hana mpango huo. Ni vyema kama mwanamke akiamua kujiingiza kwenye uhusiano, basi awe na uhusiano na mwanaume ambaye anaonekana dhahiri kuwa ni muoaji na si wa kumchezea tu, na kuingia mit...

HAKUNA NDOA ILIYOKAMILIKA ASILIMIA 1000%

Nataka kukuambia kuwa hakuna ndoa iliyo kamili yaani perfect, na kama kuna mtu Anakwambia kuwa ndoa yake ipo perfect ujue huyo ni muongo mkubwa vinginevyo kama hao watu waliooana ni mazombi kwa maana nyingine siyo Binadamu, hata kama ni ya mchungaji wako, shehe wako au hata askofu wako wa jimbo . hata hao mnaoona wanatupia mapicha picha na wake zao au waume zao kuonyesha kuwa wapo happy Haimaanishi kuwa ndio Muda wote asubuhi mpaka jioni,jumatatu mpaka jumapili, January mpaka December wao ni kucheka tu  hapana kiasi Kwamba ukaona kuwa ndoa yako haifai kabisa au upo kwenye Shimo, Kwenye ndoa watu kuna kukwazana, kupishana, hata kugombana kabisa wakati mwingine lakini  kikubwa tunachotofautiana wengi ni namna ya kushughulikia hayo matatizo yanapojitokeza na kuishia kuharibu ndoa zetu wenyewe Katikati ya ndoa yenu nani mumemweka kama mhimili wenu ni Mungu au nani,? Wanaume kujaa ufahari kuwa mimi mwanaume Bwana siwezi omba msamaha, wanawake na wao husema Kwamba atanionaje ...

HII NI MAALUMU KWA WANAUME

Wanaume wengi wanafikilia kuwa mwanamke anachohitaji kwenye maisha ni hela, magari na mijizawadi ya kumdanganyia,  lakini ukweli ni kwamba mwanamke sahihi kwako au mke wako hahitaji hivyo vyote kwani kwake hivyo ni matokeo tu katika maisha ila anachojali zaidi ni Muda wako kwake, upendo wako kwake, Kujali kwako, ukweli wako kwake, uaminifu wako kwako,  na Tabasamu, na wewe kumfanya yeye ndio kipaumbele chako na zaidi ya vyote uwe na hofu ya Mungu. Hela, magari na zawadi ni Kazi bure kama hivyo vyote vingine havioni ndani ya Nyumba kwa kuwa kwako hajafata hivyo wengine hata kwao hela zilikuwepo na hata pia hayo magari yalikuwepo na bado yapo, na walikuwa wanavitumia ila kwako kuna vya ziada alivyofata ambavyo ni muhimu zaidi kuliko hayo magari na hela. Zingatia sana kujali familia yako kwani upendo wako ni wa thamani sana kwao Kumbuka ndoa yoyote Iliyodumu au mahusiano yoyote yaliyodumu maana yake kuna mmoja Kati yao Alikuwa anajishusha, Walikuwa wanasameheana pale walipokose...

EPUKA KUJIAMINISHA JUU YA KILE AMBACHO UMEHIDIWA

asilimia kubwa yatu tupenda kujiwekea uhakika wa  kile ambacho wanakitarajia kutoka kwa watu wengine lakini kila siku nimekuwa nikisema jambo hili kwenye makala zangu za kila siku kuwa jambo hilo limewatesa wengi sana hasa pale wanapokuwa wameshindwa kupata msaada juu ya kile ambacho walitarajia. kwa mfano kuna watu wanatumia pesa vibaya kwa sababu tu kuna sehemu wameahidiwa kuwa watapata kiwango chochote cha fedha kitakachowasaidia kutimiza yale ambayo wangependa yatimie katika mipango yao. hatima ya kujiaminisha siku zote ni fedheha kwni mambo yanabadilika na maisha ya watu yanabadilika pia. kwa hiyo unashauriwa kuwa na uhakika na kile ambacho unacho mkononi kwako na siyo kilichopo kwa mtu mwingine. haijarishi ni ndugu yako , jamaa yako, rafiki nk . epuka sana kuamini kauli zao juun ya upande wa fedha ama mambo ambayo unaona kabisa wamba kutimia  kwako ni vigum .

NUKUU YA LEO

Kuishi na wanadamu kuna hitaji akili na uwezo mpana wa kutambua tabia za kila mmoja anayekuzunguka. kwa kufanya hivyo itakurahisishia wewe kujipapmbanua na kwendana na tabia zao. siyo kwa kufuata kile wanacho kiishi( ndoto zao) bali kwa kuzingatia zile tabia zao ambazo umezijifunza kutoka kwao il wasiwe sehemu ya kukwamisha mipango yako na malengo ambayo umejiwekea.  usiogope kiwango cha maneno utakayo nenewa wakati wa kuwasoma hao bali jidhatiti vya kutosha kwa kuangalia mzigo wa malengo yako uliyo nayo. kusemwa ni sehemu ndogo sana katika maisha ya mwanadamu inategemea unasemwa juu ya nini na ni kwa namna gani unaujua ukweli juu ya kile knachosemwa juu yako. lazima utambue kwamba umekuja hapa duniani kutimiza makusudi maalimu na wala siyo kwa bahati mbaya bali ni kwa mipango na maona makubwa toka kwa mwenyezi mungu aliyekupendelea uwepo hapa duniani na amekujalia uhai wa kuendelea utimiza makusudi yake hapa duniani. unaweza kuwatumia wanadamu kama sehemu ya kunufaika kwa kutum...