Skip to main content

Posts

Showing posts from 2018

USHAURI WA WADAU WA JUKWAA LETU LA TUJENGANE MEDIA

Imeandikwa na mwanamke ambaye ameachika kwa mume wake na sasa anaishi peke yake na kulea mtoto Nimeandika kwenu  ili muweze kuelewa kuwa wakati mwingine ni vema kuwathamini Wenza wetu. Nina miaka 32, Mimi na mume wangu tulikuwa kwenye mahusiano kwa Muda wa miaka 6 na tulikuwa marafiki kabla hatujaoana, nilimsubiri mume wangu mpaka alipomaliza chuo, baadaye wazazi wakafahamiana na sisi tukafunga  ndoa na sasa tuna mtoto wa miaka 7.mume wangu Alikuwa ni mtu wa kukasirika haraka  lakini hayo yote yalianza baada ya mimi mwenyewe kutaka kumuonyesha kuwa hawezi kunitawala. Kila mara tulipogombana kidogo tu nilichukua mizigo yangu na kwenda kwetu kuelezea,dada yangu anachukua simu na kuanza kumpigia simu mume wangu na kumgombeza, na nilikuwa nikimtishia kuwa kama vipi nipe talaka yangu, huku Moyoni kiukweli simaanishi kweli kutaka talaka, nilikuwa naleta tu ufahari na kutaka kutoonekana nimeshindwa au Nina shida naye sana, siku moja kwa matendo yangu nilisababisha mpaka akan...

NUKUU KUELEKEA MWAKA MPYA

Binti yoyote  utambue kuwa kuna tofauti ya kuolewa na kujioa mwenyewe, sasa usiwe na haraka mpaka ukafikia hatua ya kuamua kujioa  maana huko ndani Jasho litakutoka, Mungu Anaweza asikupe ndizi moja Leo lakini kesho akakupa mkungu mzima wa ndizi hivyo kikubwa ni kuwa na subira na imani kwa Mungu, mfano kuchangia mahari au kujilipia mahari sio jukumu lako,  kuolewa na mtu asiye na Kazi au shughuli ya kufanya halafu weee ndio umhudumie kwa kuwa una kipato na umri unaenda na wenzio wameolewa Hilo pia hapana Hilo sio jukumu lako pia wewe ndio wa kuhudumiwa na kutunzwa pale msaada wako unapohitajika sawa ndio maana ukaitwa msaidizi na sio kichwa, kuolewa tu ilimradi na wewe umetoa gundu kuwa na mimi niliwahi Vaa shera kama wengine mnavyosema hata kama unajua kuwa mwanaume hakupendi ila una mimba yake na wazazi wamelazimisha ili usiwatie aibu Nyumbani wakati unajua kabisa ndoa yako itakuwa na mtikisiko mana mume hana upendo na wewe hivyo yajayo unayajua hilo pia sio kwakuwa kun...

WANAWAKE WENGI HUFUNGA NA KUOMBA WANAUME WA NAMNA HII.

Ndugu zangu, nimeongea kuhusu baraka na heri ya kuwa na mwanamke wa pekee pia ni vizuri kwa wakina dada na wanawake kutambua kuwa nao wanatamani sana kuwa na mume wa namna hii. Hii pia ni namna moja ya sisi wanaume kujidai katika ndoa zetu. Mke huyu ana heri anapompata mume wa namna hii: 1️⃣ Mume anayemjua Mungu na anaishi maisha ya kumpendaza Mungu. 2️⃣ Mume anayetambua kuwa yeye ni baba wa familia, mume wa ndoa na mlinzi wa familia. 3️⃣ Mume anayejua kuwa mke wake anatakiwa kusikiliza na siyo kukaripia na kugombezwa kama mtoto na wakati mwengine kutamkiwa maneno makali mbele ya watoto. 4️⃣ Mume ambaye ana uwezo wa kujishusa pale anapofanya kosa, anapoumiza hisia za mke wake. 5️⃣ Mume ambaye anatambua ulimwengu wa mwanamke na anatambua mahitaji ya mke wake. 6️⃣ Mume ambaye anashirikisha mambo ya familia na ndoa kwa mke wake na wanapanga mipango mbalimbali ya familia kwa pamoja. 7️⃣ Mume ambaye anatambua kuwa ni wajibu wake kuwa na muda wa pekee wa kuwa na mke wake, kama vile ...
Kila hatua utakayopiga kwenye maisha yako lazima itakuwa na watu wa kuzungumza juu ya hatua zako. kwa maana nyingine tunasema kwamba kadiri unavyojitahidi kufanikiwa ndivyo unaongeza kiwango cha madui kwenye maisha yako. ila idadi yao haina madhara kwako kama utaamua kupuuza kile ambacho wanakisema juu yako. wapo wengine ambao hata kama ni watu wako wa karibu lazima watajinua kuyazungumzia maendeleo yako.haijarishi umekuwa ukiwasaidia kwa kiasi gani au unawasaidia kwa kiwango gani bado hahao watakugeukia na kuwa na kuwa mwiba kwenye maendeleo yako. kinachohitajika hapo ni kuwapuza na kutofanyia kazi yale ambayo unaamini kwamba yatakuwa na matokeo hasi kwenye maisah yako binafsi. endelea kuamini kuwa mabadiliko yako yapo mikononi mwako kwa sababu tunasema kijana mpumbavu atayavunja maisha yake kwa akili zake mwenyewe. jikite zaidi kwenye kutafuta mabadiliko juu ya malengo yako na mipango yako . wanadamu siku zote wema wao huwa haupo katika yale ambayo umejitoa kwa ajili yao bali we...
Moja ya ajari kubwa ambazo nakutana nazo kila siku katika mizunguko yangu ni ajari ya watu kuvunjika moyo juu ya kile amabacho waliamini kwambacho waliamini kwamba wanakiendea kwa nia njema na lazima kukifanikisha.  Nimekuwa nikiwatia moyo watu mbalimbali ambao wamepata hizi ajari za kuvunjika moyo kwa muda mrefu.  Asilimia kubwa ya watu tunashindwa kufika kule tunakoenda kimaisha kwa sababu tumejikitia tamaa mapema au wengine tumekatishwa tamaa juu ya imani tuliyojenga kwenye kitu frani.  Hii imetugarimu wengi na kufanya tukose uwelekeo kabisa wa maisha mara baada ya kushindwa kwenye hatua furani. Leo ningependa kuchukua nafasi hii kukutia moyo tena kwamba inawezekana kufikia malengo ya kile ambacho ulikuwa unafanya na kukiacha kwa changamoto ambazo ulikuwa ukipitia.  Kumbuka kwamba hakuna aliyefanikiwa kwa kuweka kando mambo aliokuwa akiamini kwamba ni sahihi na kufanya kitu tofauti na kile kirichomo nafsini mwake. Kushindwa mara kadhaa kwenye kile unachofanya ...

NUKUU YA LEO . 9/12/2018

Kuwa na Elimu kubwa haina maana kwamba unafahamu mambo yote katika ulimwengu tunamoishi.  Asilimia kubwa ya watu wamepotea kimaisha kutokana na falsafa hasi ya kwamba wapo sahihi muda wote kwa sababu tu ya Kiwango cha Elimu alichopata darasani.  Kwa ukweli usiopingika ni kwamba umehitimu Elimu ya darasani ila bado upo wazi au mweupe kabisa kwenye Elimu ya mtaani yani Elimu inayotumika zaidi kwenye maisha.  Elimu ya darasani itakusaidia kwa uchache sana kufanikisha mambo yako ila elimu ya mtaani itakuwezesha zaidi kutimiza ndoto zako kimaisha.  Kwa mfano kuna watu wamesoma na wana elimu kubwa ila bado Elimu hiyo waliopata darasani inazidi kuwatenga mbali na jamii inayowazunguka kwa kushindwa kuchanganua mambo kwa wakati. Itikadi hii inatokana na kuaminishawa kwamba sehemu pekee itakayo kusaidia wewe kumaliza matatizo yako ni darasani.  Ila ukweli usiopingika ni kwamba darasani pekee hakutoshi kumaliza matatizo yako.  Ispokuwa hata njee ya darasani yani heki...

USHAURI KWA WATOTO WA KIKE #MSIPOTEE KABLA YA KUTIMIZA MAKUSUDI MAALIMU

JINSI BINTI ANAVYO WEZA KUEPUKA KUCHEZEWA NA KUPOTEZA NDOTO ZAKE KIMAISHA  Wakati watu wawili mwanamke na mwanaume wanapokuwa kwenye kilele cha mapenzi, ni rahisi sana kila mmoja kuchunga kauli zake na kuongea yale ambayo yatamvutia mpenzi wake ili kila mmoja awe na mvuto kwa mwenzake na hivyo kuwa karibu zaidi. Hata hivyo watu wengi (hususan wanawake) wanashindwa kung'amua kwamba, katika mapenzi kila mmoja ana lake moyoni, na ni vigumu kujua mwenzako anawaza nini juu yako. Katika mahusiano mara nyingi wanawake ndio huumizwa kwa sababu wakati mwingine mwanaume anapomtaka mwanamke humpa matarajio makubwa kuhusu hatima yao ili kumvuta, lakini kumbe analo lake moyoni na hapo ndipo mwanamke hujikuta akijitolea kwa hali na mali akijua kwamba, mwenzake amempenda na wataoana wakati kumbe mwenzie wala hana mpango huo. Ni vyema kama mwanamke akiamua kujiingiza kwenye uhusiano, basi awe na uhusiano na mwanaume ambaye anaonekana dhahiri kuwa ni muoaji na si wa kumchezea tu, na kuingia mit...

HAKUNA NDOA ILIYOKAMILIKA ASILIMIA 1000%

Nataka kukuambia kuwa hakuna ndoa iliyo kamili yaani perfect, na kama kuna mtu Anakwambia kuwa ndoa yake ipo perfect ujue huyo ni muongo mkubwa vinginevyo kama hao watu waliooana ni mazombi kwa maana nyingine siyo Binadamu, hata kama ni ya mchungaji wako, shehe wako au hata askofu wako wa jimbo . hata hao mnaoona wanatupia mapicha picha na wake zao au waume zao kuonyesha kuwa wapo happy Haimaanishi kuwa ndio Muda wote asubuhi mpaka jioni,jumatatu mpaka jumapili, January mpaka December wao ni kucheka tu  hapana kiasi Kwamba ukaona kuwa ndoa yako haifai kabisa au upo kwenye Shimo, Kwenye ndoa watu kuna kukwazana, kupishana, hata kugombana kabisa wakati mwingine lakini  kikubwa tunachotofautiana wengi ni namna ya kushughulikia hayo matatizo yanapojitokeza na kuishia kuharibu ndoa zetu wenyewe Katikati ya ndoa yenu nani mumemweka kama mhimili wenu ni Mungu au nani,? Wanaume kujaa ufahari kuwa mimi mwanaume Bwana siwezi omba msamaha, wanawake na wao husema Kwamba atanionaje ...

HII NI MAALUMU KWA WANAUME

Wanaume wengi wanafikilia kuwa mwanamke anachohitaji kwenye maisha ni hela, magari na mijizawadi ya kumdanganyia,  lakini ukweli ni kwamba mwanamke sahihi kwako au mke wako hahitaji hivyo vyote kwani kwake hivyo ni matokeo tu katika maisha ila anachojali zaidi ni Muda wako kwake, upendo wako kwake, Kujali kwako, ukweli wako kwake, uaminifu wako kwako,  na Tabasamu, na wewe kumfanya yeye ndio kipaumbele chako na zaidi ya vyote uwe na hofu ya Mungu. Hela, magari na zawadi ni Kazi bure kama hivyo vyote vingine havioni ndani ya Nyumba kwa kuwa kwako hajafata hivyo wengine hata kwao hela zilikuwepo na hata pia hayo magari yalikuwepo na bado yapo, na walikuwa wanavitumia ila kwako kuna vya ziada alivyofata ambavyo ni muhimu zaidi kuliko hayo magari na hela. Zingatia sana kujali familia yako kwani upendo wako ni wa thamani sana kwao Kumbuka ndoa yoyote Iliyodumu au mahusiano yoyote yaliyodumu maana yake kuna mmoja Kati yao Alikuwa anajishusha, Walikuwa wanasameheana pale walipokose...

EPUKA KUJIAMINISHA JUU YA KILE AMBACHO UMEHIDIWA

asilimia kubwa yatu tupenda kujiwekea uhakika wa  kile ambacho wanakitarajia kutoka kwa watu wengine lakini kila siku nimekuwa nikisema jambo hili kwenye makala zangu za kila siku kuwa jambo hilo limewatesa wengi sana hasa pale wanapokuwa wameshindwa kupata msaada juu ya kile ambacho walitarajia. kwa mfano kuna watu wanatumia pesa vibaya kwa sababu tu kuna sehemu wameahidiwa kuwa watapata kiwango chochote cha fedha kitakachowasaidia kutimiza yale ambayo wangependa yatimie katika mipango yao. hatima ya kujiaminisha siku zote ni fedheha kwni mambo yanabadilika na maisha ya watu yanabadilika pia. kwa hiyo unashauriwa kuwa na uhakika na kile ambacho unacho mkononi kwako na siyo kilichopo kwa mtu mwingine. haijarishi ni ndugu yako , jamaa yako, rafiki nk . epuka sana kuamini kauli zao juun ya upande wa fedha ama mambo ambayo unaona kabisa wamba kutimia  kwako ni vigum .

NUKUU YA LEO

Kuishi na wanadamu kuna hitaji akili na uwezo mpana wa kutambua tabia za kila mmoja anayekuzunguka. kwa kufanya hivyo itakurahisishia wewe kujipapmbanua na kwendana na tabia zao. siyo kwa kufuata kile wanacho kiishi( ndoto zao) bali kwa kuzingatia zile tabia zao ambazo umezijifunza kutoka kwao il wasiwe sehemu ya kukwamisha mipango yako na malengo ambayo umejiwekea.  usiogope kiwango cha maneno utakayo nenewa wakati wa kuwasoma hao bali jidhatiti vya kutosha kwa kuangalia mzigo wa malengo yako uliyo nayo. kusemwa ni sehemu ndogo sana katika maisha ya mwanadamu inategemea unasemwa juu ya nini na ni kwa namna gani unaujua ukweli juu ya kile knachosemwa juu yako. lazima utambue kwamba umekuja hapa duniani kutimiza makusudi maalimu na wala siyo kwa bahati mbaya bali ni kwa mipango na maona makubwa toka kwa mwenyezi mungu aliyekupendelea uwepo hapa duniani na amekujalia uhai wa kuendelea utimiza makusudi yake hapa duniani. unaweza kuwatumia wanadamu kama sehemu ya kunufaika kwa kutum...

TAMBUA HILI MWANAMKE KATIKA NDOA YAKO

Wewe ni mwanamke mkuu wa familia yako. Uwe na hekima na uweledi. Panga vizuri matumizi yako. Panga bajeti ya matumizi yako kwa njia ambayo haitasababisha hasara kwa utajiri na hekima yako. Usishindane na wengine na uwaonee wivu. Kama unaona nguo nzuri imevaliwa na mwanamke, au kama unavutiwa na fanicha na vyombo ambavyo umeviona kwenye nyumba ya rafiki, usimlazimishe mumeo kununua vitu kama hivyo ambavyo vinazidi uwezo wake wa kifedha na pengine atalazimika kukopa. Je, si vema zaidi kungoja hadi hapo ambapo hali ya kipato itaruhusu au itakapopatikana akiba ya ziada ya kuwezesha kununua vitu visivyo vya muhimu? Mara nyingi ni wale wanawake wajinga na wanaojipendelea ambao hushindwa, na kuwa wabadhirifu na kutaka kushindana. Wanawake wa aina hii huwalazimisha waume zao kuingia kwenye madeni na huchoshwa na kukasirishwa na kujaribu kuridhisha matakwa yao yasiyo weza kutoshelezwa. Wakati mwingine, ufumbuzi wa aina moja tu uliopo kwa wanaume wa kutatua matatizo haya ni uamuzi wa kumtaliki ...

UMUHIMU WA KUSOMA VITABU

Ni watu wachache sana ndiyo wanaopenda na wanafahamu umuhimu wa kusoma vitabu. Watu wengi hasa waafrika hawapendi kusoma vitabu ikiwa hakuna kinachowalazimisha kufanya hivyo kama vile mtihani, kazi, n.k. Kwa hakika kuna maarifa mengi yaliyofichwa kwenye vitabu; hii ndiyo sababu  husoma au hata kuandika vitabu. Ikiwa unataka kupata maarifa na kuboresha maisha yako kwa njia ya kusoma vitabu, basi fahamu faida 15 za kusoma vitabu. 1. Hukuongezea marifa mapya Lengo kubwa linalowafanya waandishi wa vitabu kuandika vitabu ni kuweka maarifa yao kwenye maandishi. Hivyo kwa kusoma vitabu unapata maarifa mbalimbali yaliyowekwa kwenye kitabu husika. Hivi leo kuna vitabu vinavyohusu takriban kila kitu; kwa hiyo maarifa yoyote unayoyahitaji unaweza kuyapata kwenye vitabu. 2. Hukuwezesha kufikiri kwa kina Kwa hakika vitabu huongeza sana uwezo wa kufikiri. Unaposoma vitabu unafahamu mambo ambayo yatakufanya ufikiri zaidi; mara nyingine kitabu kitakuacha na maswali ambayo yatak...

JINSI IMANI YA ELIMU INAVYO WATIA WATU UMASIKINI

Ukichunguza katika jamii, utabaini kuwa sehemu kubwa ya matajiri ni wale ambao wana elimu ndogo ama hawakusoma kabisa. Katika miji na maeneo yote; wenye majengo ya maana, wenye makampuni makubwa, wenye utitiri wa malori na mabasi, wenye maduka makubwa ni wale wa "darasa la saba” au wale ambao hawakuingia darasani kabisa. 📚 Wasomi wengi wana maisha ya kawaida yaani yale ya kiwango cha kubadilisha mboga, wakijitahidi sana wanaishia kujenga nyumba za kuishi 🏡 na 🚗 magari mawili ya kutembelea (tena kwa mikopo!). Wapo wasomi wengi tu wanaoishi kimasikini, kwa lugha ya kistaarabu tunasema wana maisha ya kuungaunga. Kiukweli idadi ya wasomi walio matajiri ni ndogo sana. Lakini Umasikini wa wasomi wengi umeanzia huko shuleni na vyuoni wanakopatia usomi wao. Madarasani kuna mambo mawili wanafundishwa wasomi ambayo ndio yanayowaroga. 1.Wameelimishwa na kuaminishwa kwamba yule anaepata maswali yote kwa usahihi ndio anaonekana amefaulu. Ukikosea unahesabika kuwa u mjinga na wenyewe...

MSAADA UTOKAO KWA MUNGU JUU NA ALIYE HAI

MIAKA 2,000 hivi iliyopita, Paulo, mwandikaji wa Biblia alimfafanua Yehova kuwa “Mungu anayetoa uvumilivu na faraja.” ( Waroma 15:5 ) Kwa kuwa Biblia inatuhakikishia kwamba Yehova habadiliki kadiri wakati unavyopita, tunaweza kuwa na hakika kwamba bado Mungu anawafariji wale wanaomtumikia. ( Yakobo 1:17 ) Kwa kweli, Biblia inafunua kwamba Yehova anawafariji kwa njia mbalimbali wale walio na uhitaji. Ni njia gani hizo? Mungu anawatia nguvu wale wanaomwomba msaada kupitia sala. Pia, Mungu anawachochea Wakristo wa kweli kuwafariji waamini wenzao. Na Yehova ameweka katika Neno lake, Biblia, masimulizi yenye kutia moyo ambayo yanawatia nguvu hasa wale wanaoomboleza kifo cha mtoto. Acheni tuchunguze aina hizo tatu za faraja, moja baada ya nyingine. “Yehova Mwenyewe Akasikia” Mfalme Daudi aliandika hivi kuhusu Muumba wetu, Yehova: “Mtegemeeni nyakati zote. Mimineni moyo wenu mbele zake. Mungu ni kimbilio letu.” ( Zaburi 62:8 ) Kwa nini Daudi alikuwa na uhakika huo katika Yehova? Daudi alia...

USICHUKULIE CHUKI KWA KILA MTU

Ikiwa jamii inayokuzunguka itajinua na kukuongelea wewe katika maeneo tofauti na mienendo tofauti , ni lazima uchukue nafasi ya kujitathimini upya na kufanya toba za kila wakati juu ya hayo. wanadamu wakati mwingine huwa na taarifa za ishara ya kuharibikiwa kwako pia  mungu huwatumia wao kukufikishia ujumbe juu ya kukutaka ubadilike na uendane na kile ambacho yeye alikusudia ufanye hapa duniani. sio kwamba kila mwanadamu nayekwandama kutokna na mienendo yako anakutakia mabaya bali wengine huwa na nia njema. hupaswi kuchukia badala yake unapaswa kujielimisha juu ya hayo na kuwatumia kama wajuzaji wako.          ...................................        

JIFUNZE HILO

Katika maisha yako usikubali kufumbia macho mambo madogo madogo ukiamini kwamba yanaweza kupata ufumbuzi siku yoyote.  Hasa unapokuwa kwenye mahusiano kati yako na mwenzi wako.  Ikumbukwe kwamba jinsi unavyozidi kufuga hali hiyo ndivyo unajiweka kwenye nafasi kubwa ya kushindwa huko mbeleni.  Penda kuwa mtu wa kumaliza vitu muda huohuo ili kuipa nafasi akili yako na nafsi yako kuhifadhi mambo mapya na makubwa kwenye Safari ya kuelekea kwenye kutimiza ndoto zako.  Ukiwa mtu wa kulimbikiza mambo siku zote lazima utavuruga hasa unapofikia wakati wa mamzi. Epuka sana kumuweka mwenzi wako kwenye mabano huku ukimtegea arudie kosa ili uyaunganishe na kuyafanyia kazi kwa pamoja. Hata hivyo asilimia kubwa ya watu huchukua matatizo hayo kuwa sehemu ya maisha yao kwa sababu ya kutoelewa hilo.  Tumia muda wako vizuri na uwekeze kwenye kujielimisha zaidi juu ya hayo.  Pia unapo fanya hivyo kwa upande mwingine unakuwa unatoa nafasi kubwa kwa shetani kujipenyeza na kuk...

KUWA NA MAMZI BINAFSI

unaporuhusu  watu kuwa wamzi wa maisha yako lazima utegemee kuwa kama wao wanavyo waza. yawezekana kabisa ni marafiki zako ndugu zako na  hata jamaa zako. hii inamanisha kwamba kwa kila hatua utakayopiga kwenye maisha yako itatokana na mawazo yao au mbinu zao za kimaisha. haijarishi ni hatua chanya au hasi. Madhara makubwa ya kufanyiwa mmzi na watu wengine ni makubwa zaidi ya kile amabacho unadhania................................................................

NUKUU YA LEO NA TUJENGANE MEDIA

Katika maisha yako usithubutu kumdharau mtu yeyote kwani kuna nguvu ambayo mungu ameweka ndani yetu ambayo wengi hatuifahamu.  Ipo nguvu ya kimafanikio katika mtu huyo ambaye leo unamdharu.  Kuna usemi  usemao  hakuna ajuaye kesho yake.  Yawezekana huyo ambaye unamdharu kwa leo ndiye amebeba dhana kubwa ya mafanikio yako.  Usijione bora kuliko wengine kutokana na mali ulizonazo au Elimu,  cheo  nk. Kupanda mulima huwa ni kazi ngumu kidogo lakini kushuka mulima ni rahisi muno.  Kwa maana nyingine kushushwa kwa pigo la mwenyezi mungu ni rahisi sana.  Usipende kulazimisha
Jilazimishe kusamehe ili iwe rahisi kwako kusamehewa mbele za mungu.  Kuna badhi ya watu wanashindwa kusamehe kabisa hata pale wenzao wanapojishusha kwa kuwaomba msamaha . Jambo la kujiuliza ni moja,  Ni kwanini wao wasisamehe kama yesu mwenyewe awasamehe? . Lazima tubadilike na kuyafuata maandiko matakatifu.

NUKUU YA LEO NA TUJENGANE MEDIA

moja kati ya nyakati ngumu ambazo mwanadamu hukumbana nazo ni ule wakati ambao wanadamu wenzio hujinua katika maisha yako wewe. hasa katika wakati ambao  unaamini kwamba upo sahihi katika mtazamo fulani wa kitu amabacho unatazama wazi kwamba kinaweza kuwa na faida kubwa kiuchumi  na maendeleo yako kiujumla.  kwa mfano unafanya mamzi sahihi ya kuwa na mwenzi wako ambaye umetafakari kwa mapana kabisa na ukaona kwamba  huyu anasitahili kuwa na mimi kulingana na tabia zake pamoja na mipango yake ya kimaisha ila kutokana na imani za kwenu ukunapingwa na kuogopeshwa juu ya mwenzi wako. mira na desturi hukwamisha vikali maendeleo ya mtu na kumfanya kutmia nguvu kubwa kuishi na mtu ambaye hakutarajia kuwa naye . hii ni kutokana na mitazamo ya watu waliotulea huku wakiamininkatika ukabira kuwa ndio chachu ya uvumilivu katika ndoa. wanashindwa kutambua kwamba ndoa inamisingi  yake na pia kuna madhara makubwa ya kuchaguliwa ni mtu wa aina gani ungepaswa kuishi naye katika...

MANENO YA MUNGU NA TUJENGANE MEDIA

“Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; nao waupendao watakula matunda yake.” (Mith.18:21) Naomba kuwasilisha ujumbe maalum kuhusu matumizi ya vinywa vyetu kwa nia ya kujifunza faida na athari zake. Ni muhimu kutambua ya kwamba maneno yatokayo katika vinywa vyetu ya nguvu. Maneno mazuri yana “nguvu za uumbaji” na maneno mabaya ni kama “silaha za maangamizi”. Maandiko tuliyosoma hapa juu yanatujulisha jinsi ambavyo, nguvu za ulimi zimebeba mauti na uzima. Hebu tujihoji kwa kifupi hapa. Hivi kweli maneno yanayotoka vinywani mwetu yanazalisha matunda gani? Je! tunatumia maneno ya ndimi zetu kujenga au kuangamiza wengine? Maneno yatokayo vinywani mwetu ni ya namna gani? Yamejaa sumu ya chuki au ladha ya upendo? Yamejaa sumu ya uchungu au dawa ya baraka? Ni maneno ya lawama au kutia moyo? Ni maneno yanayotabiri ushindi au kushindwa? Maneno ni kama vifaa vya matumizi ya kutusaidia kufikia malengo ya kimaendeleo au kushusha moyo na kusababisha mkandamizo wa moyo na msongo wa mawa...

NUKUU YA LEO

katiaka maisha usisahau kuacha nafasi ya wanadamu kukumbusha juu ya matendo yako maovu unayopitia kuelekea kwenye mwisho wako. kikubwa hupaswi kulalamika na kusononeka kwa hayo unayopitia. kumbuka nyakati na siku zaja ambazo hutapata nafasi ya kuambiwa kwamba haupo sahihi kwenye maisha yako.  Tambua kwamba maneno yao hayana  madhara yoyote kwenye maisha yako bali yanakuongezea nguvu ya kusonga mbele na kufikia mwisho wako uliomwema . Moja ya vitu ambavyo ungepaswa kuomba kwa mungu ni hekima na maarifa thabiti ili uweze kufika kule unakotazamia bila mahangaiko na magumu  yoyote.

LAZIMA KUCHAGUA KUNYAMAZA.

                              MITHALI 11:12  Asiye na akili humdharau mwenziwe; Bali mtu aliye na ufahamu hunyamaza. MITHALI 17:28 Hata mpumbavu akinyamaza, huhesabiwa hekima; Akifumba midomo yake, huhesabiwa ufahamu. Changamoto kubwa tuliyonayo ni kwamba tunataka kuongea kila wakati, tunataka kujibu kila tunachokisikia, kila tunachokiona tunataka kukisemea kitu. Kuna wakati tunasikia na kukutana na mambo ambayo kiuhalisia moyo unagoma kabisa kunyamaza, unatamani ujibu, unatamani uwaambie watu yale umefanyiwa, unatamani uelezee vile umeumizwa lakini kumbe si kila jambo linatakiwa kuongelewa. Si kila ukionacho unatakiwa kukisemea kitu. Si kila usikiacho/uambiwacho ni lazima ujibu. Si kila ufanyiwacho ni lazima umwambie kila mtu. MUHUBIRI 3:1 Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu. 7 Wakati wa kurarua, na wakati wa kushona; Wakati wa kunyamaza, na wakati wa kunena; I...

KABULA YA KUTAFUTA MCHUMBA ZINGATIA MAMBO HAYA.

by   Lameck & Faustina Mtaka USIHARAKISHE . Usiharakishe na kukurupuka kutafuta mchumba kabla ya wakati muafaka.Pengine unaweza kujiuliza ni wakati upi ni muafaka kutafuta au kuwa na mchumba?ni wakati unapokuwa umekomaa kiroho, kiakili na kimwili umejitambua kikamilifu ulikotoka, mahali ulipo na unapokwenda na umetathimini kwa makini mipango na ratiba yako ya sasa na ya baadaye ndipo waweza kuchukua hatua hii mhimu katika maisha. Wengi wamepuuzia hili na kukurupuka kutafuta mchumba bila kujitathmini na kuishia kwenye uasherati na usaliti vilivyowaletea huzuni na majuto badala ya furaha na ndoa takatifu. Biblia inasema  “ Ni nani katika ninyi Kama akitaka kujenga mnara asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama kwamba anavyo vya kumalizia asije akashindwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi watu wote waonao wakaanza kumdhihaki…….” (Luka 14:28-30).   USITAFUTE MCHUMBA KWA MSUKUMO KUTOKA NJE. Usitafute mchumba Kwa kuangalizia, kushawishiwa, kuiga au kusuk...

USHAURI KWA MABINTI

Moja  ya taswira ya kutambua kesho ya mwanamke yeyote katika ndoa yake ni kutambua msimamo wa awali. wapo mabinti ambao  wamepoteza waenzi wao kwa kushindwa kuwa na msimamo katika mahusiano yao. kwa maana nyingine tunasema wanavumishwa na wimbi la watu wakupita na ambao hwana mpango wowote wa kukuaa nao kimahusiano. tathimini inaonyesha kwamba asilimia kubwa ya wanawake ambao hawajaolewa na hawatarajii kuolewa wamekumbwa na tatizo hilo kutokana na kukoswa msimamo kipindi cha ubinti wao.    Jambo la kutambua ni kwamba unaposhindwa kuwa na msimamo lazima hadhi yako itashuka na kujikuta unakuwa mtu wakimatumizi katika upande wa wanaume. ipo haja ya kubadilika kama watoto wakike ili kuweza kutoa taswira chanya ya kesho. wanaume wanachohitaji kwa sasa ni umakini na msimamo wa mwanamke na siyo urembo wa mwanamke. japo kwa sasa wamebakia wanaume wachache wanaotumia kauli ya kwamba sura ndio kila kitu.  kuna misingi maalumu amabayo unatakiwa kuitambua kama binti ili k...